Uvunjifu wa Sheria huzorotesha uchumi

PWANI-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,Kamishna Msaidizi wa Polisi Salim Morcase ametoa elimu kwa Maafisa Usafirishaji wapatao mia sita (600) wa Wilaya ya Kisarawe waliojitoleza katika ufunuguzi wa mafunzo ya udereva yanayoendeshwa na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Aliwataka maafisa usafirishaji hao kutokujihusisha na vitendo vya vurugu na uvunjifu wa Sheria na kuhakikisha wanalinda amani kwa namna yoyote ile na kuepuka vitendo vyote vya ukiukwaji wa sheria kwani kufanya hivyo kutapelekea kukosekana kwa ajira na kuzorotesha uchumi.
Aliwataka kujiepusha na matumizi mabaya ya mtandao katika kutoa taarifa za upotoshaji na kuhamasisha vurugu na vitendo vya uvunjifu wa amani bali waitumie vizuri katika kuboresha na kurahisha majukumu yao ya kila siku na kupeana taarifa za kazi.
Alitoa wito kwa vijana wa Kisarawe kujitoa kwa wingi na kwa uaminifu mkubwa kutumia fursa ya kupata elimu watakayoipata na kuweza kujisaidia kujikwamua kiuchumi kwa kujipatia kipato halali kwa kufanya kazi kwa kufuata misingi ya sheria pamoja na kuzingatia usalama wa wengine.
Naye Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani, Mrakibu Mwanadamizi wa Polisi Edson Mwakihaba aliwapongeza maafisa usafirishaji hao kwa kujitoa kwao kushiriki mafunzo hayo yanayotolewa na NIT kwa ajili ya kuwasaidia kupata mbinu na elimu juu ya kuendesha na kutumia vyombo vya moto.
Pia, aliwahakikisha kupata leseni kwa wakati kwani ni haki ya kisheria na kuwasisitiza kujiepusha na ajali zitokanazo na uzembe kwa kutofuata Sheria za Usalama Barabarani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news