Waumini wa Kanisa la Agape wapongezwa kwa kutoa mahubiri ya amani na upendo

KAGERA-Mkuu wa Polisi Wilaya ya Karagwe, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Nyandular Novemba 30, 2025 ameongea na kuwapongeza waumini wa Kanisa la Agape lililopo Kata Ndama Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera kwa kutoa mahubiri yanayozungumzia umuhimu wa amani na upendo katika taifa letu la Tanzania.
Pia, SSP Nyandular amewataka waumini kufikisha ujumbe wa kujiepusha na maandamano kwa madhehebu mengine ili kuepukana na madhara yanayoweza kutokea wakati wa maandamano.
Sambamba na hilo, SSP Nyandular amewasihi waumini kuwa watulivu siku ya Disemba 9, 2025 kwa kutojihusisha na matendo ya uvunjifu wa amani na amewataka waendelee na shughuli za uzalishaji katika familia zao ili kujiongezea kipato.
Aidha, waumini wametakiwa kutoa ushirikiano na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za watu wanaopanga, kuhamasisha au kuratibu maandamano ndani na nje ya Wilaya ya Karagwe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news