WANANCHI WA MAENEO YA VIJIJINI MILIONI 2.7 KUNUFAIKA NA MRADI WA UJENZI WA MINARA 201 YA MAWASILIANO

DODOMA-Wananchi wa maeneo ya vijijini nchini, wanaokadiriwa kufikia takribani milioni 2.7, wanatarajiwa kunufaika na huduma bora za mawasiliano kufuatia utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Minara ya Mawasiliano ya Simu Awamu ya Kumi (10), ambao mikataba yake imesainiwa hivi karibuni kati ya Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na makampuni ya mawasiliano ya simu.
Kupitia mradi huo, jumla ya minara 201 itajengwa katika kata 201 zenye vijiji 263, hususan katika maeneo ya vijijini ambayo awali yalikuwa hayana au yalikuwa na huduma hafifu za mawasiliano

Ujenzi wa minara hiyo unalenga kuongeza upatikanaji wa huduma za uhakika za simu na intaneti kwa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news