■Kasi ya kufufua mabasi yaliyopaki na kuingizwa barabarani ni kubwa
■Shehena ya vipuri muhimu tayari imeshawasili Dar
■UDART Wanachapa Kazi saa 24 Kufufua Mabasi, Mengine Mapya Yaja;
■Ng’ingo, Bosi UDART: “Hatupoi. Wateja wetu wa Dar wanastahili huduma bora"
■Wapongezwa Kutenga Mabasi Maalum ya Wanafunzi
Na Derek K. Murusuri, Mhariri wa Teknolojia
WATANZANIA wengi wanapaswa kujua kuwa BRT ya Dar es Salaam (Mwendokasi) ni mfano wa kuigwa kimataifa (global blueprint) wa usafiri wa haraka mijini, wahenga walisema, nabii hakosi heshima, isipokuwa nyumbani kwake.







