Waziri wa Ardhi,Dkt.Akwilapo akutana na RC wa Mtwara

MTWARA-Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt.Leonard Akwilapo leo tarehe 22 Desemba 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala.
Mhe.Dkt.Akwilapo ambaye yuko ziarani mkoani Mtwara amemueleza Kanali Sawala juhudi za wizara yake katika kushughulikia changamoto za sekta ya ardhi nchini.

"Sisi kama wizara tutazifanyia kazi changamoto zote za sekta ya ardhi na hapa Mtwara tayari tumeshaanza kuzifanyia kazi, lengo ni kutaka kuwaacha wananchi wetu wawe na furaha,"amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Sawala amempongeza Mhe. Dkt Akwilapo kwa kuaminiwa na Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kuteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wizara aliyoieleza kuwa ni nyeti kutokana na kugusa maisha ya kila mtu.

"Nikuahidi Mhe. Waziri sisi kama mkoa tutajitahidi kukusemea kwa yale yote mazuri unayofanya katika mkoa wetu,"amesema Kanali Sawala.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news