Wizara ya Fedha (Fungu 50) yatangazwa mshindi wa mashindano ya Uwasilishaji Bora wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2024

DAR-Wizara ya Fedha (Fungu 50) imetangazwa mshindi wa mashindano ya Uwasilishaji Bora wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2024, yaliyofanyika tarehe 4 Desemba 2025 jijini Dar es Salaam.
Ushindi huu unaifanya Wizara ya Fedha kuwa mshindi kwa mara ya tano mfululizo tangu kuanza kushiriki kikamilifu mashindano hayo mwaka 2020.

Tuzo hiyo ilipokelewa na PAT CPA Nuru Mbekenga Abdallahmed, kwa niaba ya Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, kutoka kwa Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Deogratiaus Laurent Luswetula, ambaye alikuwa Mgeni Rasmi.
Mfululizo wa mafanikio ya Wizara katika mashindano haya ni kama ifuatavyo:

2020: Nafasi ya pili

2021: Nafasi ya pili

2022: Nafasi ya kwanza

2023: Nafasi ya tatu

2024: Nafasi ya kwanza

Mafanikio haya ni ushahidi wa weledi na dhamira ya dhati ya PAT CPA Nuru Mbekenga Abdallahmed, pamoja na timu ya wataalam, chini ya uongozi mahiri wa Katibu Mkuu Dkt. Natu El-maamry Mwamba na usimamizi wa karibu wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu ambaye hivi karibuni, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alimteua kuwa Katibu Mkuu wa Wizara mpya ya Vijana, Bi. Jenifa Christian Omolo, ambao wamefanya kazi kwa bidii kubwa kuhakikisha matumizi ya fedha za umma yanafanyika kwa uwazi na kwa kuzingatia sheria na taratibu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news