TANGA-Wananchi wa Kata ya Mombo, Wilaya ya Tanga, Mkoa wa Tanga, wametakiwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuwafichua wahalifu waliopo katika maeneo yao ili kuimarisha usalama na kudumisha amani katika jamii.
Wito huo umetolewa Desemba 6,2025 na Polisi Kata wa Kata ya Mombo, Inspekta Batazari alipotoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya uhalifu, ikiwemo kutoa taarifa mapema wanapobaini viashiria vinavyoweza kuhatarisha usalama katika maeneo yao.
Inspekta Batazari amesisitiza kuwa ushirikiano baina ya wananchi na Jeshi la Polisi ni msingi muhimu wa kuimarisha ulinzi shirikishi, akiwataka wananchi kuendelea kuwa walinzi wa kwanza wa maeneo yao na kutofumbia macho vitendo vya kihalifu vinavyojitokeza.




