Ajira mpya 980 TAKUKURU kuongeza nguvu katika mapambano ya rushwa nchini-Mheshimiwa Kikwete

VERONICA MWAFISI,
ANTONIA MBWAMBO

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema ajira mpya 980 zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) zitaongeza nguvu katika mapambano dhidi ya rushwa nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Viongozi wa TAKUKURU na wadau mbalimbali wa Taasisi hiyo (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi hao mkoani Morogoro.

Mhe. Kikwete amesema hayo wakati akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba kuzungumza na Viongozi wa TAKUKURU na Wadau mbalimbali wa Taasisi hiyo wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye hafla ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa taasisi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Cate Hotel  mkoani Morogoro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa maelezo ya awali kwa Viongozi wa TAKUKURU na wadau mbalimbali wa Taasisi hiyo (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mwigulu Nchemba kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi hao Mkoani Morogoro.

Amemshukuru Mhe. Rais kwa kutoa kibali cha ajira hizo na kuwatahadharisha watumishi wa umma kutojihusisha na vitendo vya rushwa. 

"Katika kuboresha utendaji kazi wa Utumishi wa Umma nchini hatua kali zitachukuliwa kwa watumishi watakaojihusisha na vitendo vya rushwa ili kuwa na utumishi wa umma unaozingatia Taratibu, Kanuni, Sheria na Miongozo,"amesisitiza.
Viongozi wa TAKUKURU na wadau mbalimbali wa Taasisi hiyo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mwigulu Nchemba kufungua Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi hao Mkoani Morogoro.

Mhe. Kikwete ameahidi kuwa, ofisi yake itaendelea kusimamia taasisi ya TAKUKURU kwa mujibu wa Sheria na kadri ya maelekezo ya Mhe. Rais yatakavyotolewa ili kuongeza tija na kutoa haki stahiki kwa wananchi kwa maendeleo ya Taifa.

Aidha, ameishukuru Serikali kwa uwezeshaji mkubwa wa mara kwa mara katika taasisi hiyo ikiwemo rasilimaliwatu, fedha ambazo zimesaidia kujenga majengo mbalimbali ya TAKUKURU na vifaa mbalimbali vya utendaji kazi.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila amesema ofisi yake inaendelea na utekelezaji wa shughuli zake kwa mujibu wa Sheria ambapo wamedhamiria kuimarisha kwa vitendo jitihada za Serikali juu ya mapambano dhidi ya rushwa nchini kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa kwanza Kushoto) akiwa tayari kumpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mwigulu Nchemba katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi wa TAKUKURU uliofanyika tarehe 26 Januari, 2026 Mkoani Morogoro. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu Ikulu Bw. Mululi Mahendeka.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bw. Crispin Chalamila (kushoto) akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Bi. Neema Mwakalyelye (kulia) baada ya kuwasili katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2025 wa Viongozi wa TAKUKURU uliofanyika tarehe 26 Januari, 2026 Mkoani Morogoro.

Aidha, Bw. Chalamila amesema, TAKUKURU inaendelea na kazi ya kuelimisha umma mijini na vijijini kuhusu masuala ya rushwa na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya Serikali ili kuzuia vitendo vya rushwa kwa manufaa ya nchi.

Mkutano Mkuu wa mwaka wa Viongozi wa TAKUKURU hufanyika kwa lengo la kubainisha changamoto zinazowakabili katika utendaji kazi wao na kutafuta ufumbuzi wa pamoja. Mkutano huu una kaulimbiu ya “Kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu, tutimize wajibu wetu”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here