BoT yatwaa tuzo mbili na cheti Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha

TANGA-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imejinyakulia tuzo mbili pamoja na cheti cha ushiriki katika Maonesho ya Wiki ya Huduma za Fedha yaliyohitimishwa Januari 26, 2026 jijini Tanga.
Katika maonesho hayo, BoT ilitoa elimu ya fedha kwa wananchi zaidi ya 3,000, hatua iliyoiwezesha kushinda Tuzo ya Uhamasishaji na Tuzo ya Udhamini, kama kutambua mchango wake mkubwa katika kuandaa na kufanikisha maonesho hayo.

Maonesho hayo yaliyoendeshwa chini ya kauli mbiu “Elimu ya Fedha, Msingi wa Maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi” yalihitimishwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batlida Burian.
Katika hotuba yake ya kufunga maonesho hayo, aliwahimiza wananchi, hususan wanawake, kukopa katika taasisi za fedha zenye leseni ya Benki Kuu ya Tanzania ili kuepuka mikopo kandamizi kutoka kwa wakopeshaji wasio rasmi.

”Wanawake msijiingize katika mikopo yenye masharti magumu wakati Serikali kupitia taasisi za fedha zenye leseni imeweka mazingira bora ya mikopo. Hakikisha unakopa kwenye taasisi inayotambulika yenye leseni ya Benki Kuu,” amesema Balozi Dkt. Batlida.
Kupitia ushiriki wake katika maonesho hayo, BoT imeendelea kusisitiza umuhimu wa ukopaji wa malengo katika taasisi zenye leseni kama njia ya kulinda usalama wa kifedha na kuimarisha ustawi wa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here