COSOTA yasogeza mbele hafla ya mgao wa mirabaha ya tozo ya hakimiliki

NA DIRAMAKINI

OFISI ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) imetangaza kusogeza mbele hafla ya mgao wa mirabaha inayotokana na tozo za hakimiliki, ambayo awali ilipangwa kufanyika Januari 23,2026.
Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa Januari 21,2025 na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha COSOTA, taasisi hiyo imeeleza kuwa, hafla hiyo iliyokuwa inawalenga wasanii pamoja na wabunifu wa kazi za maandishi itafanyika katika tarehe nyingine itakayopangwa na kutangazwa baadaye.

COSOTA imewahakikishia wadau wote kuwa, maandalizi ya mkutano huo yanaendelea, na kwamba tarehe mpya itatangazwa mapema mara taratibu zitakapokamilika.
Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) ipo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na imeanzishwa chini ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki na 7 ya Mwaka 1999. COSOTA ilianza rasmi mwaka 2001 ikiwa na majukumu makuu mawili, usimamizi wa Hakimiliki nchini lakini pia ukusanyaji na ugawaji mirabaha. 

Kufuatia mabadiliko ya Sheria ya fedha ya mwaka 2022 (Finance Act 2022) ilitenganisha majukumu hayo na kuanzisha makampuni binafsi ya kukusanya na kugawa mirabaha nchini (CMO),ambapo kwa sasa Ofisi ya Hakimiliki imebaki kusimamia masuala ya Hakimiliki na kutoa leseni kwa Makampuni yanayohusika na kukusanya na kugawa mirabaha (CMO) pamoja na kusimamia masuala ya uharamia wa kazi za wabunifu

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here