Gavana Tutuba afika nyumbani kwa hayati Edwin Mtei jijini Arusha kutoa pole kwa familia,ndugu na jamaa

ARUSHA-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Bw. Emmanuel Tutuba, tarehe 23 Januari 2026 amefika nyumbani kwa hayati Edwin Mtei, jijini Arusha, kwa ajili ya kutoa pole kwa familia, ndugu na jamaa kufuatia msiba wa kuondokewa na Gavana huyo wa kwanza wa Benki Kuu, aliyehudumu katika wadhifa huo kuanzia mwaka 1966 hadi 1974.
Katika salamu zake za pole, Gavana Tutuba amesema kuwa, hayati Edwin Mtei alikuwa nguzo muhimu katika uanzishwaji wa Benki Kuu ya Tanzania mwaka 1966 na kwamba mchango wake hauishii katika historia pekee bali unaendelea kuonekana kupitia misingi aliyoijenga.
Ameeleza kuwa, hayati Mtei aliweka mifumo madhubuti ya usimamizi wa uchumi wa taifa, uthabiti wa sarafu ya Shilingi ya Tanzania pamoja na uanzishaji wa mifumo ya malipo iliyoimarisha sekta ya fedha nchini.
Gavana Tutuba amesisitiza kuwa misingi hiyo imeendelea kuiongoza Benki Kuu ya Tanzania katika kutekeleza majukumu yake ya msingi, huku akieleza kuwa taifa litaendelea kumuenzi Hayati Edwin Mtei kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here