Mwinjilisti Temba aibua hoja mpya ushindi wa Ruto uchaguzi ujao Kenya

NAIROBI-Mwinjilisti wa Kimataifa kutoka Tanzania, Dkt. Alphonce Boniface Temba amesema, Mungu amempa ujumbe maalum unaomhusu moja kwa moja Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Dkt.William Ruto, akidai kuwa ujumbe huo unabeba hatima ya rais huyo kurejea madarakani katika uchaguzi ujao nchini Kenya.
Akizungumza kuhusu ujumbe huo leo Januari 23,2025, Dkt.Temba ameeleza kuwa, Rais Ruto akimpa nafasi awasilishe ujumbe huo mapema, Mungu anakwenda kumuinua kwa viwango vingine.

Pia, amesema, Rais Ruto anapaswa kumheshimu Mheshimiwa Kalonzo Musyoka, akisisitiza kuwa mchango wake ulikuwa wa msingi katika ushindi wake kwenye uchaguzi uliopita.

Aidha, Dkt. Temba amesema wakati wa uchaguzi uliomuingiza madarakani Rais Ruto, aliitwa kushiriki maombi yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kenyatta (KICC), ambako baada ya maombi hayo Mungu alimfunulia mambo ambayo Raila Odinga alipaswa kuyatekeleza ili kushinda uchaguzi.
Hata hivyo, kutokana na kushindwa kufanikisha kukutana na Raila,baada ya maombi alifanikiwa kuonana na Kalonzo Musyoka nje ya ukumbi ili aweze kumfikia Odinga,lakini alimpuuza na kumzuia.

"Kalonzo nikakutana naye pale nje, nikamwambia yapo mambo nimwambie Raila ayafanye haraka sana, ili aweze kutangazwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya,nisipokutana na Raila hatatangazwa kuwa Rais wa Kenya, atatangazwa Ruto.
Mwinjilisti Temba baada ya kupokelewa na kukabidhiwa kadi ya mwaliko na Katibu wa Mheshimiwa Raila, Andrew Mondoh katika ofisi zao zilizoko Capital Hill Square, 4th Floor Upperthil, Nairobi.Soma kwa kina hapa》》》

"Kalonzo akakataa kabisa na akanifokea sana, akasema over my ded body, kesho saa nne, Raila Odinga atatangazwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya.

"Nikamwambia, Mungu ameniambia Raila hatashinda kama sitaonana naye hatashinda na yeye aliniita,Kalonzo alikataa, Mheshimiwa Ruto unaweza kumuuliza Kalonzo, je baada ya yale maombi pale KICC hakuna mtumishi wa Mungu kutoka Tanzania alikuambia, ukakataa ndiyo mimi.

"Kwa hiyo aliyekusababisha ukawa Rais, Mheshimiwa Ruto ni Kalonzo, kama Raila angesikia maneno ya Mungu na angeyatimiza leo hii usingekuwa Rais."
Kwa mujibu wa Dkt. Temba, hatua ya Kalonzo kumzuia yeye wakati huo kumfikishia Raila Odinga ujumbe aliopewa na Mungu ilichangia kuchelewa kwa tangazo la matokeo na hatimaye kumpa ushindi Dkt.William Ruto.

Aidha,kwa mujibu wa Dkt.Temba, Kalonzo alimhakikishia kuwa Raila Odinga angekuwa ametangazwa mshindi ifikapo saa nne asubuhi ya siku iliyofuata, lakini alisisitiza kuwa bila Raila kusikia na kutekeleza ujumbe huo, asingeshinda uchaguzi huo.

Amesema kuwa, baada ya sakata hilo kupita, Mungu sasa amemtuma rasmi kukutana na Rais Ruto ili kumuombea na kumkabidhi ujumbe unaolenga kuvunja vikwazo vya kiroho vinavyodaiwa kuwepo Ikulu ya Kenya, ili awe huru na kufanikiwa tena katika uchaguzi ujao.

"Mheshimiwa Rais Dkt.William Ruto, Mungu amenituma kwako, kuongea na wewe kwa sababu ya Uchaguzi unaokuja, ambapo utawania awamu ya pili, una asilimia 50 na nina asilimia 50, namba yangu ya mawasiliano ni +255 655 973 787. Tukionana nitakuombea na niweze kukupa ujumbe na maneno ya Mungu uweze kushinda kwa urahisi."
Dkt. Temba, ambaye amewahi kuwa mshauri wa kiroho kwa marais mbalimbali barani Afrika, amesema amekuwa akialikwa na viongozi hao kwa ajili ya kuwashauri na kuwaombea, jambo ambalo, kwa mujibu wake, liliwawezesha kufanya vizuri zaidi katika uongozi wao.

Ameongeza kuwa, si mara ya kwanza kufika Kenya, akieleza kuwa wakati wa uongozi wa Rais Mwai Kibaki, Mungu alimpeleka Ikulu ambako alikutana na baadhi ya maafisa wakuu akiwemo Mdaura na Stephen Kirogo, waliompatia muongozo wa kumuombea Rais Kibaki akiwa madarakani.

Dkt. Temba amesema,Mungu amempa ujumbe maalum anaopaswa kuuwasilisha kwa Rais Dkt. William Ruto ili kuhakikisha anafanya vizuri zaidi katika uchaguzi ujao.
Pia,ameongeza kuwa,kwa nyakati tofauti amewahi kuwasilisha ujumbe wa Mungu na kufanya maombi kwa viongozi wa mataifa mbalimbali ya Afrika, ikiwemo Zambia, Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Msumbiji na Malawi, jambo ambalo, kwa mujibu wake, liliwaletea mafanikio zaidi katika uongozi wao.

Hata hivyo, Mwinjilisti wa Kimataifa,Dkt.Temba ameweka wazi wito wake wa kukutana na viongozi wakubwa duniani alioupata mwaka 2000 akiwa jijini Gaborone nchini Botswana kwa mwaka mzima haukuwa rais kukubalika katika baadhi ya Ikulu kwa sababu ya ujumbe kutozoeleka.

Mfano ni utabiri aliofikisha mwaka 2004 kwa hayati Levy Patrick Mwanawasa katika Ikulu ya Lusaka kuwa angeshinda uchaguzi wa mwaka 2006,lakini asingedumu madarakani kama asingemuombea tena.

Aidha, alimtabiria Rais wa sasa Zambia,Hakainde Hichilema kuwa endapo atamfanyia maonbi maaalumu atadumu katika Ikulu ya Zambia, ambapo kupitia Mwenyekiti wa chama chake,Steven Katuka baada ya rais kusikia akukubali maombi na wala kuishi Ikulu.

Kutokana na hali hiyo, mpaka sasa Rais wa Zambia anakaa nyumbani kwake jijini Lusaka, hii ikiwa ni kama moja ya vikwazo anavyokutana navyo Dkt.Temba katika kuwasilisha jumbe za kinabii kwa viongozi wa mataifa mbalimbali.

Mheshimiwa Hichilema hakukubali maombi ya Dkt.Temba wala kuishi Ikulu mpaka sasa na kuweka historia kwa rais wa kwanza nchini Zambia kugoma kuhamia Ikulu kutokana na maonyo ya mtumishi wa Mungu.
Aidha, pamoja na Nabii kutokupata heshima nyumbani, haikuwa hivyo kwa Mwinjilisti Dkt.Temba katika maandamano ya baada ya uchaguzi 2025 Tanzania.

Kwani, Dkt.Temba aliibuka hadharani kupiga maombi kwa Mungu na kuwasii GenZ wasiandamane Desemba 9,2025 ambapo watu zaidi ya milioni 24 duniani waliona na maandamano yakakoma hadi leo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here