Manchester City imekamilisha rasmi usajili wa mshambuliaji Antoine Semenyo kutoka AFC Bournemouth baada ya kufikia kifungu cha kuvunja mkataba wake chenye thamani ya pauni milioni 65.
Semenyo, mwenye umri wa miaka 26, amesaini mkataba wa muda mrefu wa miaka mitano na nusu utakaomuweka ndani ya Etihad Stadium hadi mwaka 2031. Usajili huo unaufanya kuwa wa kwanza kwa Manchester City katika dirisha hili dogo la usajili.
Man City wamewashinda wapinzani wao wakubwa Manchester United, Liverpool, Tottenham Hotspur na Chelsea, ambazo pia zilikuwa zikihitaji saini ya mshambuliaji huyo kutokana na kiwango chake bora msimu huu.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

















