BARAZA la Mitihani Tanzania (NECTA) limefuta matokeo ya wanafunzi 89 waliohusika na udanganyifu na kuandika matusi katika karatasi zao wakati wa upimaji wa kitaifa wa darasa la nne na kidato cha pili.
Soma matokeo ya Kidato cha Pili na Darasa la Nne 2025 hapa》》》
Hayo yamebainishwa jijini Dar-es-Salaam Januari 10, 2026 na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani, Profesa Said Mohamed, wakati akitagaza matokeo ya kitaifa ya darasa la nne na kidato cha pili iliyofanyika Oktoba na Novemba 2025.
Soma matokeo ya Kidato cha Pili na Darasa la Nne 2025 hapa》》》
Amesema wanafunzi 41 walifanya udaganyifu na nane waliandika matusi kwenye skripti zao katika upimaji wa kitaifa wa darasa la nne huku wanafunzi 29 walifanya udaganyifu na 11 waliandika matusi kwenye skripti zao katika upimaji wa kitaifa wa kidato cha pili.Soma matokeo ya Kidato cha Pili na Darasa la Nne 2025 hapa》》》
“Hatua hii imechukuliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5(2)(j) cha Sheria ya Baraza la Mitihani, Sura ya 107, kikisomwa pamoja na Kifungu cha 30(2)(b) cha Kanuni za Mitihani za mwaka 2016,” amesema Profesa Mohamed.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo













