Magazeti leo Januari 9,2026

SERIKALI imeendelea kuchukua hatua za kimkakati katika kuimarisha mfumo wa upatikanaji wa haki nchini, baada ya Wizara ya Katiba na Sheria kuingia makubaliano mapya ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) pamoja na Shirika la Legal Services Facility (LSF), yenye lengo la kupanua huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi.
Akizungumza Januari 8,2026 Mtumba jijini Dodoma wakati wa utiaji saini wa hati za ushirikiano baina ya pande hizo tatu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Eliakim Maswi,ameeleza kuwa ni hatua muhimu katika mageuzi ya sekta ya haki, hususan kwa wananchi wa kipato cha chini na makundi maalumu yanayohitaji ulinzi zaidi wa kisheria.

Bw.Maswi alisema kuwa, utiaji saini huo si tukio la kawaida, bali ni hatua yenye uzito wa kisera, kikatiba na kiutendaji inayolenga kuondoa vikwazo vya kimfumo vinavyowakwamisha wananchi kupata haki kwa wakati.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here