Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na mabenki ya biashara, imefanikiwa kuvunja genge la kimataifa la wahalifu wa kifedha lililokuwa likijihusisha na wizi wa taarifa za kadi za benki na utakatishaji fedha nchini.
Uchunguzi ulioanza Mei 2025 umebaini watuhumiwa kutoka mataifa mbalimbali wakiwamo raia wa China na Watanzania, huku waathirika wa uhalifu huo wakitoka mataifa 11 yakiwamo Marekani, Canada, Japan na Australia.
Fedha zilizoibwa zilikuwa zikitolewa bila ridhaa ya wahusika na kutumika kulipia huduma mbalimbali nchini.
Imeelezwa kuwa, zaidi ya shilingi bilioni 18 zilitakatishwa kati ya mwaka 2022 hadi 2025, huku watuhumiwa zaidi ya 137 wakikamatwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Kilimanjaro na Zanzibar.
Tayari mashauri yamefunguliwa mahakamani na zaidi ya shilingi bilioni 4 zimerejeshwa au kuzuiwa.
TAKUKURU imesisitiza kuwa, hatua za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi ya wahusika wote waliobainika kuhusika na mtandao huo wa kihalifu.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo





















