NA DIRAMAKINI
JKT Tanzania imeendelea kujijita kileleni ma msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa alama 17 baada ya mechi 10 huku Yanga SC ikiwa nafasi ya pili kwa alama 16 baada ya mechi sita.
Kwa mujibu wa msimamo uliotolewa leo Januari 17,2026 na Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania, nafasi ya tatu inashikiliwa na Pamba Jiji yenye alama 16 baada ya mechi tisa.
Aidha,nafasi ya nne inashikiliwa na Mashujaa FC kwa alama 13 baada ya mechi tisa huku Simba SC ikiwa nafasi ya tano kwa alama 12 baada ya mechi tano
