DODOMA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM -TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewaongoza viongozi na watumishi wa ofisi hiyo, kupanda miti katika viwanja vya OWM- TAMISEMI Mtumba, ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyeadhimisha siku yake ya kumbukukumbu ya kuzaliwa kwa kupanda mti katika eneo la Bungi Kilimo, Mkoa wa Kusini Zanzibar.
Akizungumza na watumishi mara baada ya zoezi la kupanda miti Prof. Shemdoe ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa nchini kuandaa mpango endelevu wa upandaji miti katika mikoa yao, na kuwataka kuhakikisha Mamlaka za Serikali za Mitaa zinautekeleza mpango huo kwa ufanisi.
Akizungumza na watumishi mara baada ya zoezi la kupanda miti Prof. Shemdoe ametoa wito kwa Wakuu wa Mikoa nchini kuandaa mpango endelevu wa upandaji miti katika mikoa yao, na kuwataka kuhakikisha Mamlaka za Serikali za Mitaa zinautekeleza mpango huo kwa ufanisi.“Tunapanda miti hii,lakini tunawajibu wa kuihudumia na kuitunza, kila aliyepanda mti ahakikishe haufi, binafsi nitakuwa naufuatilia mti wangu na kuunyeshea maji ili ukue vizuri, na wito wangu kwenu nanyi mfanye hivyo hivyo,” ameeleza Prof. Shemdoe.
Katika zoezi hilo la upandaji miti, Prof. Shemdoe ameungana na Manaibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Dkt. Jafar Seif na Mhe. Reuben Kwagilwa, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Bw. Sospeter Mtwale, Wakuu wa Idara na Vitengo na baadhi wa watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI katika kuadhimisha siku hiyo ya kumbukukumbu ya kuzaliwa ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Januari 27 ameendeleza utamaduni wa kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kupanda miti, ambapo leo amepanda mti eneo la Bungi Kilimo, Mkoa wa Kusini Zanzibar na kuahidi kuendelea na utamaduni huo huku akiwataka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuendelea kusimamia upandaji wa miti katika maeneo yaliyoathirika.






