Magazeti leo Januari 3,2026

SERIKALI imekamilisha kufunga mifumo ya kunasa radi katika shule 12 zilizopo wilayani Bukombe mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya kuwalinda wananchi pamoja na wanafunzi dhidi ya ajali za radi.
Hatua hiyo inakuja kufuatia mfululizo wa matukio ya radi wilayani humo ikiwemo tukio la Januari 27, 2025 lililopelekea vifo vya wanafunzi saba na kujeruhi 82 katika Shule ya Sekondari Businda.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Pasikasi Muragili ametoa taarifa hiyo katika mahojiano na waandishi wa habari na kueleza kuwa maboresho yanaendelea kabla ya shule kufunguliwa Januari 13, 2026.

Muragili amesema ili kufanikisha mpango huo serikali kupitia halmashauri hiyo imeweka mkakati wa kutenga fedha kidogo kidogo kila mwezi kwa ajili ya uwekaji wa mifumo ya kunasa radi.

Amesema mbali na maeneo ya shule serikali pia imeshatoa maelekezo kwa taasisi za umma na kijamii ikiwemo taasisi za kidini kuchukua hatua ya kuweka mifumo hiyo kwenye maeneo yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here