MATAIFA nane yamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 inayoendelea kupigwa nchini Morocco.
Michezo ya robo fainali itaanza kuchezwa Januari 9, 2025, ambapo Mali itachuana vikali na Senegal, huku wenyeji wa mashindano hayo, Morocco, wakivaana na Cameroon.Ratiba itaendelea Januari 10, 2025 kwa michezo miwili mingine ya robo fainali, ambapo Algeria watamenyana na Nigeria, huku Misri (Egypt) wakiwakabili mabingwa wa watetezi wa kombe hilo, Côte d’Ivoire. Washindi wa michezo hiyo watainga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

















