Mheshimiwa Abdullah akutana na Balozi wa Urusi nchini Tanzania

ZANZIBAR-Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah amekutana na kuzungumza na Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey Avetisyan aliyemtembelea Ofisini kwake Zanzibar kwa ziara ya kikazi tarehe 26 Januari,2026.
Viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa uwili na kutilia mkazo kuimarisha Utalii, Nishati, Elimu na Utamaduni na uhusiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya Tanzania na Urusi.

Katika mazungumzo hayo Mhe. Hemed Suleiman Abdullah amesisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iko tayari kuhakikisha mazingira wezeshi kwa wawekezaji kutoka Urusi wanaokwenda kuwekeza visiwani Zanzibar.
Naye Balozi Avetisyan ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa utayari wake wa kuimarisha biashara na uwekezaji kati ya Urusi na Tanzania.

Ametoa wito kwa SMZ kushiriki kikamilifu katika vikao vya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano wa Kibiashara na Kiuchumi kati ya Urusi na Tanzania.

Awali Mheshimiwa Balozi Avetisyan alikutana na kuzungumza na Kaimu Mkurungenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar Bw. Ali Suleyman Ali katika Ofisi hiyo.
Katika kikao hicho wamebadilishana mawazo kuhusu utekelezaji wa mipango ya pamoja na kukubaliana kuendelea na mashauriano kuhusu masuala ya ushirkiano wa uwili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here