ANTONIA MBWAMBO,
VERONICA MWAFISI
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Serikali kupitia Ofisi yake imetekeleza ahadi ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuajiri vijana 12,000 ndani ya siku 100 za kwanza za kipindi cha pili cha awamu ya sita.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026. Wengine ni Viongozi na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI.
Waziri Kikwete amesema hayo wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Januari 30, 2026 katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026.
Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliahidi kuajiri vijana 5,000 kwa sekta ya Afya na watumishi 7,000 kwa sekta ya elimu ambao ni Walimu wa Masomo ya Sayansi na Hisabati.
Mhe, Kikwete alisema kuwa hadi tarehe 20 Januari, 2026 watumishi hao wapya wamepatikana na wamepangiwa vituo na barua za ajira zimetumwa moja kwa moja kwenye akaunti za waombaji hao na wamesharipoti katika vituo vyao vya kazi.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray akifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa Waziri huyo na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026.
“Kwa sasa mambo yote yanakwenda kidijiti ambapo watumishi hao wapya wamepokea barua zao za ajira kwa njia ya simu za mkononi na wameripoti kwenye vituo vyao vya kazi na waliowahi kabla ya kutuma taarifa za mishahara wamepokea mshahara wao wa kwanza mwezi huu wa Januari,” Mhe. Kikwete aliongeza.
Aidha Mhe. Kikwete ametoa wito kwa waajiriwa wapya ambao bado hawajaripoti katika vituo walivyopangiwa kufanya hivyo ndani ya siku 14 tangu walipopokea barua ya kazi, kinyume na hapo nafasi zao zitachukuliwa na wasailiwa wengine ambao wapo katika kanzi data.
Mh. Kikwete ametoa wito kwa Vijana wa kitanzania kuwa kwa wale wote wenye sifa wasisite kuomba nafasi za ajira pindi zitakapotangazwa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwani Serikali bado itaendelea kutangaza nafasi hizo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitazama makala maalum kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO mara baada ya kuzungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026. Katikati ni Naibu Waziri wake Mhe. Regina Qwaray na wakwanza kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Bw. Juma Mkomi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray (wa kwanza kulia) akifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa Waziri huyo na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026. Wengine ni Viongozi na Watendaji wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora.
Mwandishi wa Habari kutoka gazeti la Uhuru, Bw. Fred Alfred (aliyeshika kipaza sauti) akiuliza swali kuhusu ajira wakati wa Mkutano wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026.
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bw. Mick Kiliba (wakwanza mstari wa mbele kulia) akifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa siku 100 za ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Ukumbi wa Habari-MAELEZO jijini Dodoma leo tarehe 30 Januari, 2026. Wengine ni Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora.
Kadhalika Mhe. Kikwete amesema, katika kutekeleza ahadi za siku 100 za Mhe. Rais, Dkt Samia Suluhu Hassan, Ofisi ya Rais, Menejiementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeboresha Mfumo wa kielektroniki wa e-Mrejesho ambapo Wananchi wanaweza kuwasilisha maoni au malalamiko kupitia mfumo huo ili kuimarisha Utawala Bora.
Mhe. Kikwete amehitimisha kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa maelekezo ya kuhakikisha vijana wanapata ajira ili kuongeza wigo wa kutoa huduma kwa umma.




