Mheshimiwa Ndejembi ahimiza ushirikiano kwa wakuu wa mikoa na wilaya utekelezaji wa miradi ya nishati

DODOMA-Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi leo Januari 22, 2026, amezungumza katika Mkutano wa Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa Mwaka wa Fedha 2024/25 unaofanyika katika Ukumbi wa Mabeyo, jijini Dodoma.
Mkutano huo umeandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na umewahusisha Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Maafisa Lishe kutoka mikoa yote nchini.
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri Ndejembi amewasihi Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa karibu katika utekelezaji wa miradi ya nishati inayotekelezwa katika maeneo yao, ili kufanikisha azma ya Serikali ya kusogeza huduma bora za nishati kwa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here