PWANI-Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Bw. Crispin Francis Chalamila amekabidhi mashine mbili za watoto waliozaliwa kabla ya muda kwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Pwani (Tumbi).
Akizungumza katika makabidhiano hayo Januari 20, 2026, Bw. Chalamila amesema, mashine hizo zimepatikana kwa michango ya watumishi wa TAKUKURU nchi nzima katika kujitoa kwa jamii katika matendo ya huruma, lengo likiwa ni kutoa mashine hizo kwa kila mkoa Tanzania Bara.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Januari 20, 2026, Bw. Chalamila amesema, mashine hizo zimepatikana kwa michango ya watumishi wa TAKUKURU nchi nzima katika kujitoa kwa jamii katika matendo ya huruma, lengo likiwa ni kutoa mashine hizo kwa kila mkoa Tanzania Bara.Akizungumza kuhusu takwimu za watoto wanaopokelewa na kuruhusiwa kurudi nyumbani wakiwa na afya njema kutoka hospitali ya Tumbi, Dkt. Adelina Rutashobya ambaye ni Daktari Bingwa wa watoto hospitalini hapo alisema, asilimia 16 ya watoto wanaopokelewa hospitalini hapo wanapoteza maisha.
Takwimu hizi zinaonesha ni kwa kiasi gani mashine hizi mbili zilizotolewa na TAKUKURU zitasaidia kuokoa maisha ya watoto waliozaliwa kabla ya muda yaani chini ya wiki ishirini na nane (28).
Aidha Dkt. Amani Malima ambaye ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Pwani (Tumbi) kwenye neno la shukrani alisema "Kwa kiasi kikubwa mashine hizi tulizozipokea kutoka kwa watumishi wa TAKUKURU zitaokoa maisha ya watoto wengi wenye uhitaji. Hakika tunawashukuru sana."
Awali Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU alielezea kuwa, tangu Desemba mwaka 2024 mkoani Arusha ambapo TAKUKURU walitoa msaada wa mashine hizo kwa mara ya kwanza, walipata hamasa ya kuendelea kujitolea kama matendo ya huruma kwa jamii na kuahidi kuwafikia watoto nchi nzima kwa kutoa mashine katika hospitali za rufaa za mikoa yote.

