Mkutano wa Kikanda wa Kukabiliana na Uvuvi Haramu na Kukuza Uchumi wa Buluu kufanyika Zanzibar

NA DIRAMAKINI

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la Ascending Africa kupitia Mradi wa Jahazi, inatarajia kuandaa Mkutano wa Kikanda wa Kukabiliana na Uvuvi Haramu na Kukuza Uchumi wa Buluu, unaolenga kuimarisha ushirikiano wa kikanda katika usimamizi endelevu wa rasilimali za baharini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, Kapteni Hamad Bakar Hamad, mkutano huo unalenga kuimarisha uongozi wa Afrika katika usimamizi wa bahari, kukuza uchumi wa buluu unaozingatia uendelevu, pamoja na kuimarisha hatua za pamoja za kukabiliana na uvuvi haramu katika ukanda wa Kusini-Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIO).

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, mkutano huo wa siku tatu utafanyika kuanzia tarehe 26 hadi 28 Januari, 2026 na utawakutanisha wawakilishi wa serikali, taasisi za kikanda, wadau wa sekta ya bahari, wataalamu wa masuala ya baharini pamoja na washirika wa maendeleo kutoka Mauritius, Kenya, Tanzania na Zanzibar.

Imefafanuliwa kuwa, mkutano huo unaakisi vipaumbele vya pamoja vya nchi za ukanda wa SWIO ambazo zinakabiliwa na changamoto za matumizi endelevu ya rasilimali za baharini, usalama wa chakula, mabadiliko ya tabianchi pamoja na ustawi wa jamii za pwani.

Kupitia mkutano huo wa Blue Voices 2026, nchi washiriki zinalenga kujenga mwitikio wa kikanda unaojikita katika ushirikiano wa dhati, uwazi wa mifumo ya usimamizi wa bahari, pamoja na utekelezaji madhubuti wa sera, sheria na mikakati ya bahari.

Aidha, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesisitiza kuwa changamoto zinazokabili bahari katika ukanda wa SWIO haziwezi kutatuliwa na taifa moja pekee, bali zinahitaji mshikamano wa kikanda. 

Kupitia uongozi wake katika kuandaa mkutano huo, Zanzibar inalenga kuimarisha diplomasia ya bahari, kukuza ushirikiano wa kikanda na kuweka msingi wa hatua za pamoja dhidi ya uvuvi haramu.

“Zanzibar imejidhatiti kushirikiana kwa karibu na nchi jirani katika kulinda bahari yetu ya pamoja. Mkutano wa Blue Voices 2026 unatupa jukwaa muhimu la kuimarisha mshikamano wa kikanda, kuendeleza suluhu za vitendo na kuongeza ufanisi wa mapambano dhidi ya uvuvi haramu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here