Msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara leo Januari 18,2026

NA DIRAMAKINI

BODI ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPLB) leo Januari 18,2026 imetangaza msimamo wa ligi baada ya kuchezwa michezo mbalimbali ya Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2025/2026, ambapo timu ya JKT Tanzania inaendelea kushika nafasi ya kwanza.

Kwa mujibu wa msimamo huo, JKT Tanzania imekusanya pointi 17 baada ya kucheza mechi 10, ikishinda michezo minne, sare tano na kupoteza mchezo mmoja, hali inayoiweka kileleni mwa msimamo wa ligi.

Nafasi ya pili inashikiliwa na Young Africans SC (Yanga SC), ambayo imecheza mechi sita na kujikusanyia pointi 16, ikifuatiwa na Pamba Jiji katika nafasi ya tatu pia ikiwa na pointi 16 lakini ikizidiwa kwa tofauti ya magoli.

Mabingwa watetezi Simba SC wapo nafasi ya nne wakiwa na pointi 13 baada ya michezo sita, sawa na Mashujaa FC waliopo nafasi ya tano kwa idadi hiyo hiyo ya pointi, huku Azam FC ikishika nafasi ya sita ikiwa na pointi 12.
Aidha,katika msimamo wa katikati ya jedwali, Namungo FC, Mtibwa Sugar, Fountain Gate na TRA United SC zinaendelea kupambana kujiimarisha katika msimamo huo huku zikitenganishwa na tofauti ndogo ya pointi.

Mbeya City, Tanzania Prisons na Dodoma Jiji zinaendelea kuburuza mkia,huku KMC FC ikishika nafasi ya mwisho kwa pointi nne baada ya kucheza mechi tisa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here