NAIROBI-Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa, Dkt. Alphonce Temba amemuomba Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Dkt.William Ruto kuitisha maombi ya Kitaifa ili kila Mkenya aweze kumlilia Mungu aliokoe Jiji la Nairobi dhidi ya vitendo vya ukahaba ambavyo vinaendelea kuharibu taswira ya jiji hilo lenye hadhi ya kipekee ya kiuchumi.
Dkt.Temba ameyasema hayo usiku wa kuupokea mwaka mpya 2026 baada ya kukumbana na kisa kilichomshangaza cha mama ambaye anajihusisha na ukahaba jijini humo na kuamua kumfanyia maombi ya ukombozi.
"Leo ni tarehe moja mwezi wa kwanza 2026, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, William Ruto huyu ni mama ambaye nimemsikia nikiwa kwenye hoteli akilia karibu masaa matatu, anamlilia Mungu amtoe kwenye hii madhabau ya ukahaba.
"Nimekuja Nairobi miaka 10 iliyopita, Nairobi ni moja ya miji iliyojengeka vizuri, Nairobi ni moja ya miji ambayo Wakenya ni wafanyabiashara na ni watafutaji wazuri, lakini wanawake wa Nairobi wamekamatwa na madhabau ya ukahaba.
"Madhabau ya ukahaba inawatesa, hivyo Mheshimiwa Rais itisha maombi ya Kitaifa...itisha maombi ya Kitaifa kila mtu atoke ndani amlilie Mungu wake ili roho ya ukahaba ikafe katika jina la Yesu."
Aidha, Dkt.Temba baada ya kumfanyia maombi ya ukombozi mama huyo anayejiuza jijini Nairobi alimpatia shilingi 5,000 ya Kenya ambayo ni zaidi ya shilingi 100,000 ya Kitanzania na kumtaka aachane na biashara hiyo na kwenda kuanzisha biashara ndogo japo ya kutembeza mboga mtaani na Mungu kupitia sadaka hiyo atamtendea maajabu makubwa.
Katika shughuli hiyo ya ukahaba wanawake hao huwa wanaanzia shilingi 300 ya Kenya kwa kujiuza ambayo ni sawa na shilingi 2,000 za Kitanzania.
Aidha, mara nyingi huwa hawapati kitu kutokana na dhuluma za kingono ambazo hufanyiwa na wateja wao, hivyo mama huyo alimshukuru Dkt.Temba kwa kumfanyia maombi ya ukombozi na kumpatia mtaji.
Mwinjilisti Dkt.Alphonce Boniface Temba unaweza kumpata kupitia WhatsApp namba +255655973787. Huyu ni miongoni mwa watumishi wachache wa Mungu ambao wamekirimiwa neema za kipekee na ya ajabu na amekuwa akifanya mambo makuu.
Kwa uchache, Dkt.Temba amekuwa akiwatabiria na kuwaombea marais barani Afrika ambapo tayari marais nane wamepata huduma yake.
Vilevile, Mungu amekuwa akimtumia kufanya mambo makubwa katika huduma ndani ya mataifa 12 barani Afrika na matukio mengi makubwa yasiyo ya kawaida Mungu amekuwa akimtumia kuyatenda na kufanyika baraka kwa jamii na mataifa mbalimbali.
Kwa sasa, Dkt.Temba yupo jijini Nairobi kwa ajili ya kazi za kiroho na Mungu ameendelea kumtumia kwa viwango vikubwa.
