DAR-Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne iliyofanyika Novemba, 2025 ambapo ufaulu umeongezeka kidogo.
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Said Mohamed ametangaza matokeo hayo jijini Dar es Salaam leo Januari 31, 2026 ambapo amesema kuwa,ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.62 kulinganisha na ufaulu wa mwaka 2024.
Pia, amesema takwimu zinaonesha kuwa ufaulu wa jumla umepanda kwa asilimia 2.61 na hivyo kufikia asilimia 94.98 ambapo watahiniwa 526,620 wamefaulu kwa kupata dvision I, II, III, na IV, mwaka 2024 watahiniwa waliofaulu walikuwa 477,262 sawa na asilimia 92.37 na mwaka 2023 walikuwa 471,427 sawa na asilimia 89.36.
CLICK ANY LETTER BELOW TO FILTER CENTRES BY ALPHABET |
