DAR-Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limefuta matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne kwa wanafunzi 77 kutokana na makosa ya udanganyifu na matumizi ya lugha chafu wakati wa mtihani.
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Profesa Said Mohamed ameyasema hayo leo Januari 31,2026 jijini Dar es Salaam wakati akitangaza matokeo hayo.
Amesema,kati ya wanafunzi hao, 47 walibainika kuhusika na udanganyifu wakiwa katika vituo vya mitihani, huku wanafunzi 30 wakitokea shuleni.
Profesa Mohamed amesema,baadhi ya wanafunzi walihusika na vitendo vya kuandika lugha isiyo na staha kwenye karatasi za majibu, hali ambayo ni kinyume na kanuni na miongozo ya mitihani ya taifa.
Amesisitiza kuwa, baraza halitasita kuchukua hatua kali dhidi ya yeyote atakayekiuka taratibu za mitihani, akibainisha kuwa lengo ni kulinda uadilifu, haki na ubora wa elimu nchini.Soma matokeo zaidi hapa
