NIRC na JKT zaungana kuongeza uzalishaji kupitia Umwagiliaji

MOROGORO-Shamba la Chita JKT, lenye ukubwa wa ekari 12,000 zinazolimwa, limepangwa kuwa mfano wa ushirikiano kati ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC).
Tangu mwaka 2021, Jeshi limekuwa likiendeleza mashamba haya kwa kutumia rasilimali za ndani, likikodisha mitambo na kusawazisha mashamba ili kuongeza tija ya uzalishaji wa mpunga.

Katika ziara yake ya hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa NIRC, Bw. Raymond Mndolwa, ametembelea maeneo ya mito yenye miundombinu ya kupeleka maji mashambani na kukutana na uongozi wa JKT katika skimu hiyo na kutoa maagizo mahsusi ya kuimarisha skimu hiyo na kuahidi kuchukua hatua za haraka ndani ya siku 14, lengo likiwa ni kuijengea uwezo CHITA JKT katika uzalishaji wa mazao.
Bw. Mndolwa amesisitiza kuwa upo umuhimu wa kutafuta mbinu ya uhifadhi wa maji, ikiwemo kujenga mabwawa, ili maji mengi yanayopotea yaweze kuhifadhiwa na kutumika kwa Umwagiliaji.

“Kunauhitaji wa kujengwa bwawa jipya, lijengwe kwa kutumia maji kutoka Mto Monyo, ili kusaidia kilimo cha mpunga na shughuli nyingine za matumizi ya maji kwa Chuo cha Jeshi kilichopo eneo hilo,”amesema.

Mndolwa ameongeza kuwa,kutokana na changamoto za usawazishaji wa mashamba, usanifu utafanyika upya kwa kushirikisha wataalamu wa Jeshi, NIRC na Mshauri Elekezi

“Ndani ya siku 14, usanifu huo upitiwe ili kuboresha ujenzi unaoendelea na kubaini vyanzo vipya vya kujenga mabwawa,” ameongeza Mndolwa.

NIRC ipo tayari kuendelea kushirikiana na Jeshi la kujenga Taifa, kuhakikisha hekari zote 12,000 zinamwagiliwa ipasavyo, na bajeti itatengwa mara usanifu utakapokamilika.
Amesisitiza kuwa, maboresho ya vyanzo vya maji na upanuzi wa mashamba katika eneo hilo la JKT ni sehemu ya mpango wa muda mrefu wa NIRC wa kuongeza tija ya uzalishaji katika kilimo cha Umwagiliaji na kwamba hatua hizo zinalenga kulifanya Shamba la Chita JKT kuwa mfano wa kitaifa wa kilimo cha kisasa, sambamba na malengo ya Dora 2050 na Mpango wa Maendeleo wa Miaka 5 wa serikali.

Naye Afisa Tawala wa Jeshi la Kujenga Taifa, Brigedia Jenerali Hassan Rashid Mabena, alisifu hatua ya NIRC kupitia Mkurugenzi Mkuu Mndolwa, kwa kutembelea na kujionea shughuli zinazofanywa na Jeshi na kuchukua hatua za haraka.

Amesema,ushirikiano huo utaliwezesha Jeshi kufikia malengo yake ya kuongeza uzalishaji wa mazao na kutatua changamoto zinazojitokeza.
Ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa NIRC imeweka mwelekeo mpya wa kimkakati kwa Shamba la Chita JKT, kutoka kilimo kinachotegemea rasilimali za ndani, kuelekea kilimo cha Umwagiliaji chenye mabwawa ya kudumu na mashamba yaliyosawazishwa kitaalamu.

Ushirikiano wa NIRC na Jeshi unatarajiwa kufanya Chita JKT kuwa nguzo ya uzalishaji wa mpunga na mazao mengine nchini Tanzania na mfano wa ushirikiano wa kitaifa katika sekta ya Umwagiliaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here