ZANZIBAR-Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar imetoa muongozo mpya kuhusu utaratibu wa shughuli za misiba, baada ya kupokea malalamiko na kubaini kuwa muongozo wa awali kwa vikundi vya kinamama vinavyohitimisha, uliotolewa Oktoba 26, 2023, haukuwa ukifuatwa ipasavyo.
Kutokana na hali hiyo, ofisi hiyo iliwaita tena wahitimishaji katika kikao kilichofanyika Januari 13, 2026, ambapo baada ya kufanya mazungumzo ya kina, iliamua kutoa muongozo mpya utakaozingatiwa kuanzia sasa.
Muongozo huo unaelekeza yafuatayo:
1. Muhitimishaji apewe idhini au mwaliko rasmi kutoka kwa familia ya wafiwa wenyewe.
2. Kusimamishwa kwa michango ya aina zote katika misiba (mazishi).
3. Michango inayohusu wafiwa isimamiwe na familia husika pekee.
4. Kusimamishwa kwa aina zote za biashara katika maeneo ya misiba.
Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar imesisitiza kuwa muongozo huu uanze kufuatwa kuanzia tarehe ya leo, na imewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa pale wanapoona utaratibu huo haukuzingatiwa.
Wananchi wametakiwa kuwasilisha taarifa kupitia namba ya simu 0778 426 474 ili hatua stahiki zichukuliwe.
Tags
Breaking News
Habari
Muongozo wa Mazishi Zanzibar
Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar
Zanzibar News


