Polisi Jamii wahimizwa kuimarisha ushirikiano na jamii kudhibiti uhalifu

MOROGORO-Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Elisante Ulomi kwa kushirikiana na Mkaguzi wa Polisi, Ezron Magesa kutoka Makao Makuu ya Polisi Dodoma Kamisheni ya Polisi Jamii wametoa elimu kuhusu Ushirikishwaji wa Jamii katika kutanzua na kubaini uhalifu, kukuza uzalendo pamoja na kuimarisha usalama, amani na utulivu kwa Maafisa Polisi Jamii wa Mikoa ya Morogoro, Singida, Iringa na Dodoma leo Januari 5, 2025.
Katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Polisi Mkoa wa Morogoro, mada mbalimbali ziliwasilishwa zikilenga kuongeza uelewa kwa Maafisa hao juu ya mbinu shirikishi katika ulinzi wa raia na mali zao kupitia dhana ya Polisi Jamii. Washiriki walipata fursa ya kujadili namna bora ya kuelewa mazingira ya jamii inayowazunguka, kutambua tabia za wananchi na kutumia taarifa hizo kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu.
Watoa mada hao wamesisitiza kuwa ushirikiano wa karibu kati ya Polisi na wananchi ni nguzo muhimu ya kujenga mazingira salama. Wamehimiza Maafisa Polisi Jamii kuwa chachu ya mabadiliko kwa kutoa elimu endelevu kwa jamii ili kuhamasisha uwajibikaji wa pamoja katika kudhibiti uhalifu na kuendeleza utulivu katika maeneo yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here