ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameizindua rasmi Barabara ya Chake–Wete (km 22.2), akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwekeza katika miundombinu ili kuifungua Pemba kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi.
Rais Dkt. Mwinyi amesema miundombinu ni msingi wa maendeleo ya haraka, akitaja miradi mikubwa inayoendelea Pemba ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Pemba, Bandari za Mkoani na Wete, pamoja na barabara kuu za Mkoani–Chake na Chake–Wete.
Amesisitiza wananchi kuacha kujenga katika hifadhi za barabara, huku akihakikishia waliotoa maeneo yao kupisha miradi ya maendeleo kulipwa fidia stahiki.
Barabara hiyo imejengwa na Kampuni ya MECCO, kwa gharama ya Shilingi Bilioni 26.6, kwa ufadhili wa BADEA na Saudi Fund.

















.jpg)


