Zanzibar imefanikiwa kujitosheleza katika uzalishaji kuku-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar sasa imefanikiwa kujitosheleza katika uzalishaji wa kuku, hatua itakayopunguza utegemezi wa uagizaji wa kuku kutoka nje ya nchi.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Januari 8,2026 alipofungua rasmi Mradi wa Shamba la Ufugaji wa Kuku wa Zan Breed Limited, akisisitiza kuwa uwekezaji huo mkubwa lazima uwanufaishe wafugaji wadogowadogo kupitia elimu, vifaranga bora, chakula cha kuku, huduma za chanjo na masoko ya uhakika.
Ameuelezea mradi huo kuwa wa kimkakati na wa kimataifa, unaoonesha uwezo wa Zanzibar kuanzisha na kuendesha miradi mikubwa ya uzalishaji wa ndani, huku akisisitiza umuhimu wa sera za kifedha na kodi zitakazolinda wawekezaji na viwanda vya ndani.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameiagiza Wizara ya Uwezeshaji na Wizara ya Kilimo kuhakikisha wafugaji wadogowadogo wanawezeshwa kupitia mikopo isiyo na riba, mafunzo na masoko, na kuutumia Mradi wa Zan Breed kama msingi wa kuwawezesha wafugaji kote Zanzibar.
Kwa mujibu wa ZIPA, mradi huo una mtaji wa Dola za Marekani Milioni 105, unatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 1,000 na una uwezo wa kuzalisha kuku 800,000 kwa mwezi, pamoja na huduma za kliniki ya kuku, kiwanda cha nafaka, maabara na mfumo wa kuchakata maji, hatua itakayochochea kwa kiasi kikubwa maendeleo ya sekta ya mifugo na uchumi wa Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here