Rais Dkt.Mwinyi aitaka misikiti iwe kitovu cha utatuzi wa changamoto katika jamii

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi, amewasisitiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuitumia misikiti kama vituo muhimu vya kujadili na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii, sambamba na kutoa ufumbuzi unaofaa kwa maendeleo ya jamii.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Januari 23,2025 baada ya kujumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa wa Mfereji wa Wima, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema kuwa, changamoto zilizopo katika jamii ni nyingi, hivyo ni wajibu wa waumini kushirikiana kupitia misikiti kwa kuhamasisha michango itakayosaidia familia na jamii duni zisizojiweza.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amepongeza uongozi wa Msikiti wa Mfereji wa Wima kwa kuanzisha na kuendesha utaratibu wa ukusanyaji wa michango kwa ajili ya kusaidia wahitaji.

Katika kuunga mkono jitihada hizo, Rais Dkt. Mwinyi ameahidi kuchangia Shilingi Milioni 34 kwa ajili ya kuimarisha mfuko wa msikiti huo, huku akiwahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kutoa michango yao kwa moyo wa kujitolea ili kuwasaidia wenzao wenye uhitaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here