Simba Queens yaongoza Ligi Kuu ya Wanawake baada ya michezo 10

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Simba Queens imeendelea kuonesha ubora wake katika Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (WPL) msimu wa 2025/2026 baada ya kuongoza msimamo wa ligi kufuatia michezo 10 ya mwanzo.
Simba Queens wanaongoza ligi wakiwa na pointi 28, baada ya kushinda mechi tisa na kutoka sare moja bila kupoteza mchezo wowote.

Timu hiyo imefunga mabao 21 na kuruhusu mabao mawili pekee, hali inayoonesha uimara mkubwa wa safu yao ya ulinzi na ushambuliaji.

Nafasi ya pili inashikiliwa na Yanga Princess wenye pointi 24 baada ya kucheza mechi tisa, wakifuatiwa na JKT Queens walioko nafasi ya tatu wakiwa na pointi 20.
Pia, Alliance Girls wanashika nafasi ya nne kwa pointi 19, huku Fountain Gate Princess wakikamilisha tano bora kwa pointi 16.

Kwa upande wa chini ya msimamo wa ligi, hali si shwari kwa Bilo FC na Ruangwa Queens ambao wanashika nafasi mbili za mwisho.

Ruangwa Queens wapo mkiani wakiwa na pointi tatu baada ya kupoteza mechi tisa kati ya 10 walizocheza.

Aidha,Ligi Kuu ya Wanawake inaendelea kupamba moto huku ushindani ukiwa mkali katika nafasi za juu na chini ya msimamo wa ligi, kila timu ikipambana kusaka pointi muhimu kadri msimu unavyoendelea.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here