Rais Dkt.Mwinyi aiweka Zanzibar kwenye Ramani ya Juu ya Utalii duniani

NA DIRAMAKINI

ZANZIBAR chini ya uongozi unaoacha alama wa Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi imeendelea kuimarika kama kitovu muhimu cha utalii duniani,baada ya kushuhudia ongezeko kubwa la wageni wa kimataifa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Takwimu zinaonesha kuwa, idadi ya watalii wanaotembelea visiwa hivyo imeongezeka kwa kasi kuanzia mwaka 2020 hadi 2025, hali inayoashiria mafanikio makubwa ya sekta ya utalii.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi, mwaka 2020 Zanzibar ilipokea watalii 260,644. Idadi hiyo iliongezeka hadi 394,185 mwaka 2021, kabla ya kupanda zaidi mwaka 2022 kufikia watalii 548,503.

Aidha,mwaka 2023 uliweka rekodi mpya ya wageni 638,498, huku mwaka 2024 ukishuhudia ongezeko hadi watalii 736,755.

Mafanikio makubwa zaidi yameonekana mwaka 2025, ambapo Zanzibar imepokea jumla ya watalii 910,682 wa kimataifa, ikiwa ni ongezeko kubwa zaidi katika historia ya hivi karibuni ya sekta hiyo.

Ongezeko hilo linatajwa kuchangiwa na maboresho ya miundombinu, sera madhubuti za kukuza utalii, kuimarika kwa usalama, pamoja na jitihada za kimkakati za kuitangaza Zanzibar kimataifa kama kituo bora cha utalii wa fukwe, historia, utamaduni na burudani.

Kutokana na mafanikio hayo, Zanzibar chini ya Rais Dkt.Mwinyi imetambuliwa kimataifa kama moja ya maeneo bora ya utalii duniani, hali inayochochea ukuaji wa uchumi, ajira kwa wananchi na kuimarika kwa mapato ya Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here