NA DIRAMAKINI
UWEKEZAJI Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi katika Sekya ya Elimu umeendelea kuleta matokeo chanya, ambapo mwaka 2025 Zanzibar imeandika historia kwa viwango vya juu vya ufaulu wa mitihani ya Kidato cha Pili (93.2%) na Darasa la Nne (94.0%).
Mafanikio haya yametokana na miundombinu bora ikiwemo skuli za ghorofa za msingi na sekondari,ajira za walimu, pamoja na uboreshaji wa vifaa vya kujifunzia ikiwemo maabara za kisasa,maktaba za kisasa na vyumba vya kompyuta.
Vilevile, kwa matokeo hayo ufaulu wa Skuli za Vipawa kwa Wanafunzi wa Kidato cha Pili wa Skuli za Fidel Castro na Lumumba wamepata Daraja la Kwanza wote asilimia 100%.
Hatua hizi zinaonesha dhamira thabiti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha elimu na kuandaa kizazi chenye maarifa na ushindani.
