ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaachia huru wanafunzi 17 wa Chuo cha Mafunzo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar tarehe 12 Januari 2026.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.
Msamaha huo umetolewa kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 59 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kinachompa uwezo wa kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyehukumiwa kwa kosa lolote.
Katika msamaha huo, wanafunzi 17 waliokuwa wakitumikia adhabu mbalimbali wameachiwa huru, ambapo wanafunzi 11 wametoka Unguja na wanafunzi 6 kutoka Pemba.
Hatua hii ni sehemu ya utaratibu wa kawaida ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi hutumia maadhimisho ya kitaifa kutoa msamaha kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo.

