Rais Dkt.Mwinyi atunuku Nishani za Mapinduzi kwa viongozi na wananchi wenye sifa maalum

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametunuku Nishani ya Mapinduzi pamoja na Nishani ya Utumishi Uliotukuka kwa viongozi na wananchi mbalimbali wenye sifa maalum, waliotoa mchango mkubwa katika historia, maendeleo na ustawi wa Zanzibar.
Akisoma Tamko la Kwanza la Kutunuku Nishani hizo, Katibu Mkuu wa Afisi ya Rais, Ikulu Zanzibar, Ndg. Saleh Juma Mussa, amesema jumla ya watu 18 wametunukiwa Nishani hizo, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao wa kipekee kwa Taifa.
Hafla hiyo imefanyika leo Januari 11,2026 katika Viwanja vya Ikulu, Mnazi Mmoja Zanzibar, na imehudhuriwa na viongozi wa kitaifa, viongozi wa vyama vya siasa, watendaji wakuu wa taasisi za umma, wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama, pamoja na wananchi mbalimbali.

Tukio hilo ni miongoni mwa shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Waliotunukiwa Nishani ya Mapinduzi ni pamoja na:









Waliotunukiwa Nishani ya Utumishi Uliotukuka ni pamoja na:










Nishani ya Mapinduzi hutolewa kwa mtu aliyeasisi, kushiriki au kuyatukuza Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, au kwa kiongozi, mtu aliye hai au aliyefariki aliyeiletea Zanzibar heshima na sifa katika fani mbalimbali, pamoja na kuonesha maadili mema yanayostahili kuigwa.

Kwa sasa, Wazanzibari wanaendelea kuadhimisha Miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia shamrashamra na mat

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here