Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Uwanja wa Gombani pamoja na Fainali za Mashindano ya Mpira wa Miguu Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup).
📅 13 Januari, 2026
⏰ Saa 8:00 Mchana
📍 Uwanja wa Gombani, Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini – Pemba
Karibu tushuhudie tukio muhimu la kihistoria katika kuendeleza michezo na miundombinu ya michezo Zanzibar.
