NA DIRAMAKINI
TIMU ya Taifa ya Senegal imeibuka mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 leo Januari 18,2026 baada ya ushindi wa kishujaa katika mchezo wa fainali dhidi ya Morocco, ikithibitisha ubora na uimara wake katika soka barani Afrika.
Katika dimba la Prince Moulay Abdellah Stadium uliopo Rabat nchini Morocco, Papa Gueye dakika ya 94 aliiwezesha Senegal kuandikisha rekodi ya kipekee katika michuano hiyo mikubwa barani Afrika.
Ushindi huo unaifanya Senegal kuendelea kujiimarisha kama moja ya mataifa yenye nguvu katika mchezo huo, huku kikosi chake kikionesha nidhamu, umoja na kiwango cha juu cha kiufundi katika mashindano yote.

