Serikali imetoa onyo kwa waajiri na wafanyakazi wa sekta binafsi kuhakikisha kima cha chini cha mshahara kinatekelezwa ipasavyo.
Hayo yamebainishwa Januari 16, 2025 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Clement Sangu wakati akitoa ufafanuzi kuhusu Amri ya Kima cha Chini cha Mshahara kwa Sekta Binafsi.
Mhe. Sangu amesema amri ya kima cha chini cha Mshahara kwa Sekta Binafsi imeanza kutumika kuanzia tarehe 1 Januari, 2026 na ilitangazwa kupitia Gazeti la Serikali la tarehe 13 Oktoba, 2025 ambapo kima cha chini cha Mshahara kimeongezeka kwa asilimia 33.4.
Amesema, zoezi la mapitio ya kima cha chini cha Mshahara lilikuwa shirikishi ambapo Serikali kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri na Vyama vya Wafanyakazi walikubaliana utekelezaji wake.
“Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kushirikiana na waajiri, wafanyakazi pamoja na Vyama vayo ili kuhakikisha mazingira ya kazi na hali za wafanyakazi zinaboreshwa ili kukuza tija na ustawi wa wafanayakazi,” amesema.
Tags
Front Pages
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Newspapers
Newspapers Today
Yaliyojiri Magazetini Leo























