Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa, lingependa kutoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa zisizo sahihi zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zinazodai kuwa, wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakati wakipanda miti Wilayani Nkasi wamevamiwa na mabavu kutumika kuwatawanya na kuwakamata.
Jeshi la Polisi linapenda kuufahamisha umma kuwa, taarifa hizo si za kweli zina lengo la kupotosha na kuzusha taharuki zisizo na msingi kwani katika Wilaya ya Nkasi na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla hakuna tukio la Kuvamiwa, matumizi ya mabavu wala wafuasi wa CHADEMA waliokamatwa.Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa linaendelea kuimarisha usalama wa raia na mali zao na tunaendelea kusisitiza wananchi kupuuza taarifa zinazoandaliwa na kusambazwa kwa lengo la kupotosha, kuchonganisha, kujenga chuki baina ya wananchi na taasisi mbalimbali.
Imetolewa na;
Mkoa wa Rukwa