Taasisi ya Cornwell Tanzania yaja na Mtaala wa Tiba Asili nchini

DAR-Wataalam wa kutoka Chuo cha Taasisi ya Cornwell Tanzania wamekutana na Baraza la Tiba Asili Nchini na kufanya uwasilishaji wa mtaala wa kutoa mafunzo ya tiba kwa njia za asili nchini.
Wataalamu wa Taasisi ya Cornwell Tanzania wamewasilisha mtaala huo Wizara ya Afya kwa lengo la kupata mchango na maoni ili kuboresha mtaala huo unaotarajia kuanza kutumika katika kuandaa wanafunzi wa tiba za asili.
Mwasilishaji na mtayarishaji wa mtaala huo Dk. Fredrick Mukebezi amesema mtaala huo utajikita zaidi katika kuandaa maarifa na kujenga kujiamini kwa wanafunzi ili waweze kuwa bora katika kujenga uwezo na uelewa tofauti na wanafunzi wengi wanaotumia kigezo cha kufaulu mtihani tu.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa kikao kazi hicho leo Junuari 26, 2026 Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Asili Wizara ya Afya, Dkt. Winfrida Kidima amesema, tayari mtaala huo umepitishwa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET).
Kiongozi huyo amesema kuanzishwa kwa mafunzo hayo ni hatua muhimu sana kwa upande wa Tiba Asili nchini nakuwapongeza viongozi wa Taasisi hiyo kwa kuanzisha mafunzo hayo.

Naye Mtendaji Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Elizabeth Lema kutoka Cornwell Tanzania amesema chuo chake ni cha pili Afrika na kubainishwa kuwa mafunzo haya pia yanatolewa na Chuo kilichopo nchini Afrika ya kusini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here