DODOMA-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, aliyefika kwa ajili ya kujitambulisha na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo kati ya Tanzania na Japan, katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Treasury Square jijini Dodoma. .jpg)
.jpg)
Katika kikao hicho Mhe. Balozi Omar, aliishukuru Serikali ya Japan kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Tanzania na kupongeza ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya nchi hizo mbili, akisisitiza dhamira ya Serikali ya kuendelea kufanya kazi kwa karibu na washirika wa maendeleo ili kuhakikisha miradi inayotekelezwa inaleta tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini, Mhe. Yoichi Mikami, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kuimarisha mazingira mazuri ya ushirikiano na Japan, hasa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayolenga kukuza uchumi, miundombinu na ustawi wa wananchi, sambamba na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika maeneo ya kipaumbele.Kikao hicho kilihudhuriwa pia Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Kaimu Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera, Wizara ya Fedha, Dkt. Remidius Ruhinduka, Wakuu wa Idara wasaidizi na maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.








.jpg)
.jpg)
.jpg)