Rais Dkt.Mwinyi ahimiza maadili,elimu na mshikamano katika jamii

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewanasihi Waumini wa Dini ya Kiislamu kutenda mambo mema ili kutajwa kwa wema ndani ya jamii pale wanapotangulia mbele ya haki.
Alhaj Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo Januari 16,2026 alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyosaliwa katika Msikiti wa Bamita Chumbuni, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Dkt. Mwinyi amesema Serikali imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini kote, ikiwa ni juhudi za Serikali kuhakikisha inatimiza matarajio makubwa ya wananchi.
Naye Katibu Mtendaji wa Afisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume, ametoa wito kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kutafuta elimu zaidi ili kujijengea heshima ndani ya jamii.

Msikiti wa BAMITA uliwekewa jiwe la msingi na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi mwaka 1981.
Alhaj Dkt. Mwinyi anaendelea na utaratibu wake wa kujumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa kwa kusali katika misikiti mbalimbali mijini na vijijini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here