DAR-Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesitisha vyeti na leseni 106 za kutumia alama ya ubora ya TBS kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo maombi ya kufunga biashara.
Sambamba na kutokutii masharti ya leseni kwa mujibu wa Kanuni ya 28 ya Kanuni za Usajili wa Majengo na Uthibitishaji wa bidhaa, 2021 (The Standards (Registration of Premises and Certification of Products) Regulations, 2021).TBS imeutaka umma kuepuka kununua au kusambaza bidhaa zilizositishiwa kutumia alama ya ubora ya TBS na kutoa taarifa endapo watabaini bidhaa hizo zipo sokoni.
Orodha kamili ya vyeti na leseni zilizositishwa hii hapa chini;




