DAR-Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeufungia Uwanja wa KMC uliopo Dar es Salaam kutumika kwa michezo ya ligi, kwa sababu haujakidhi vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu.
Taarifa ya TFF imeeleza kuwa,miundombinu ya uwanja huo haikidhi masharti yaliyowekwa katika kanuni za leseni za klabu.
Kutokana na uamuzi huo, timu zinazotumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani zitalazimika kuhamia uwanja mwingine hadi pale uwanja wa KMC utakapofanyiwa marekebisho na kukaguliwa tena na TFF.
Uwanja huo ulianza kutumika kwa michezo ya usiku.TFF pia imezikumbusha klabu zote kuendelea kutunza na kuboresha miundombinu ya viwanja.
