KILIMANJARO-Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Januari 24, 2026 amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ambapo anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika mazishi ya marehemu Mzee Edwin Mtei, yanayofanyika Tengeru jijini Arusha.
Mzee Mtei ambaye aliwahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika kipindi cha mwaka 1966 hadi 1974 alifariki usiku wa Januari 19, 2026 jijini Arusha.
